Thursday, June 21, 2012

AJALI DAR


Breaking News:Ajali yaua sita Dar

Habari iliyotufikia chumba cha habari cha Globu ya Jamii hivi punde,inaeleza kuwa watu watatu wamepoteza maisha papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali iliyokutanisha magari mawili iliyotokea hivi sasa maeneo ya Tegeta Kibaoni njia panda ya kwenda Wazo Hii jijini Dar.
Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni Lori lililokuwa likitokea Wazo Hill ambalo lilikuwa kwenye mwendo kasi kufeli breki na kwenda kugonga gari la abiria likikokuwa limesimama hapo Kibaoni kupakia abiria.
Shughuli ya kuokoa majeruhi kwenye ajali hiyo inaendelea hivi sasa.
Wadau,
Ule usemi ya kwamba unapokuwa unaendesha barabarani na mbele yako kuna daldadala ni sawa na kwamba unaendesha magari mawili, nimeuamni leo hii asubuhi pale njia panda ya Tegeta kwenda Wazo kiwanda cha Cement wakati ambapo Daladala alipomchomekea jamaa mwenye Rav 4 MPYA akaingia mtaroni na daladala kukimbia.
Mdau
Mbando



  BY REHEMA



 




 

Tuesday, June 19, 2012

TRIPOLI YAANGUKA; MWISHO WA GADDAFI?


 

Ndani ya masaa 72 Jiji la Tripoli nchini Libya limeanguka mikononi mwa waasi ambao walikuwa wanaendesha kampeni ya kumuondoa rais wa nchi hiyo Dikteta Muammar Gaddafi. Kuanguka kwa jiji la Tripoli kunaashiria kuhitimishwa kwa kampeni hiyo iliyozidi kwa miezi sita kamili sasa na ambayo imegharimu maisha ya mamia ya wananchi wa Libya ambao wamekuwa chini ya utawala wa Gaddafi na familia yake kwa zaidi ya miaka 40 sasa.
Mwishoni mwa juma waasi wa Libya walikuwa wanalizunguka jiji hilo la Afrika ya Kaskazini kama fundo la kamba na pole pole waliteka maeneo mbalimbali na kuzima majaribio yoyote ya utetezi wa wapiganaji wa Gaddafi. Kusika siku ya Jumamosi jioni kuamkia Jumapili waasi walikuwa kilomita chache kutoka Viwanja vya Kijani ambapo wiki kadha wa kadha mashabiki wa Gaddafi walikuwa wakikutana kutiana shime.
Maelfu ya wananchi wa Libya wakipepea bendera ya waasi – ambayo ni bendera ya zamani ya Mfalme wa Libya – walianza kujitokeza barabarani kuwapokea waasi hao na usiku wa kuamkia Jumatatu hii maelfu zaidi wamejitokeza katika mitaa na viunga vya Jiji la Tripoli kuwakaribisha waasi hao ambao wanapigana chini ya uongozi wa Baraza la Mpito la Libya ambalo linawakilisha serikali mbadala ya ile ya Gaddafi. Hadi hivi sasa nchi 32 zimetambua baraza hilo kuwa mwakilishi halali wa wananchi wa Libya. Tanzania siyo mojawapo. (more…)

Watanzania 108 warudishwa toka Afrika Kusini




Watanzania 108 wamerudishwa Nchini wakitokea Afrika Kusini baada ya kukamatwa huko wakiishi kinyume cha sheria.
Habari zilizothibitishwa na maofisa Uhamiaji wa Tanzania, zimeeleza kwamba Watanzania hao wamewasili leo na hadi usiku huu walikua wanakaguliwa kuthibitisha uraia wao.

Tanzania yamtimua nchini raia wa Uingereza

SERIKALI kupitia Idara ya Uhamiaji, imewatimua nchini wahamiaji 26 akiwamo Raia mmoja wa Uingereza mwenye asili ya Afrika Magharibi, Fikra Pevu imethibitisha.
Uchunguzi wa Fikra Pevu, umebaini kuwa wahamiaji yao wametimuliwa nchini kwa kupewa hati ya wasiotakiwa nchini (PI) katika msako wa kushitukiza uliokuwa ukifanyika na Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam. (more…)

Prince Charles kutembelea Tanzania Nov 6


Mwana wa Malkia wa Uingereza – Prince Charles of Wales – anatarajiwa kutembelea Tanzania kuanzia Jumapili akitokea Afrika ya Kusini ambako ameanza ziara ya siku nane katika bara la Afrika. Prince Charles ambaye ni mrithi wa kiti cha ufalme wa Uingereza ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili.
Katika ziara yake hiyo Prince Charles ameambatana na mkewe Duchess of Cornwell Camilla Parker. Ziara ya Tanzania itaanza tarehe 6 hadi tarehe 9 na ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Tanganyika (eneo la Tanzania Bara) ilipata uhuru wake kutoka Uingereza iliyokuwa inaitawala kwa agizo la Umoja wa Mataifa ambapo Uingereza ilitakiwa iiandae Tanganyika kuwa huru.
Mara ya mwisho kwa Prince Charles kutembelea Tanzania katika ziara rasmi ilikuwa ni 1984 na Bi. Parker hajawahi kutembelea Tanzania. Prince Charles ndiye baba yao Prince William na Prince Harry na mke wake wa kwanza Princess Diana (mama yao William na Harry) alikufa katika ajali ya gari mwaka 1997.

HUJUMA kwa Siyoi Arumeru…. Hujuma kwa Chama chetu

Mzee Salaam,
Najua huwa unapitia hapa ukikwanguiwa kule Facebook, au “Mtuitui” anakujuza yanayoendelea, ila mchunge sana, ni mnafiki huwa anakumwagia porojo na umbeaumbea tu sanasana siku akiwa anasaka pesa za kujirusha. Mie sichapi umbea ..maa yake hawachelewi sema weka source.. source si ndio hii hapa au wewe unataka ipi tena..we-mbaba unamambo..!!
Mzee unakumbuka kilipotemwa kikao cha KK cha mwisho na kwa  rungu tukagandamizia Siyoi for Arumeru, Siyoi for the Party, na baadae ukapokea msg kutoka kwa “kiraka” kwamba MC alikuwa anachonga mbovu nje ya kikao kwamba kwa mtaji huu ni bahati kushika nafasi ya pili au tatu kwa chama letu kwenye kinyang’anyiro hicho cha Ubunge, huko kwa Wameru kutokana na sababu walizozungumzia zungumzia wajumbe za vijiubabe, vijiubabe na kama kuburuzana flan-hivi, dhana iliyookea kule Dodoma wakati wa kupitisha ile karata ya mabadiliko ya katiba ……… ila ukapuuzia kamsemo kake, nadhani sasa kuna sababu ya kuanza Tathimini kwanini Tumeshindwa.
Werevu hawasubiri mavuno ndipo wafanye tathimini, wapumbavu husubiri hadi nukta ya mwisho ya tone la mvua ndipo huamka kwamba mwaka huu ni wa njaa na kukurupuka kuomba msaada.
Kuna Uzi unatembea Chini kwa Chini wa Kukiangamiza Chama, ni HUJUMA iliyokamilika yenye Lengo la Kukomoana na kulipizana Visasi. Ukweli usemwe hata kama unauma.. look here..
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye ndiye aliyezindua kampeni za CCM Arumeru Mashariki
1.       Wakati Benja akifungua kampeni, kule Igunga alielezea kwa madaha jinsi Serikali kupitia chama letu ilivyoleta maendeleo ya miundombinu ya Barabara, Toka Dar hadi Igunga ni lami, Chama letu limefanikisha kufungua matawi ya benki (NMB) Igunga ambapo sasa wananchi wanaweza kukopa na kuweka vijisenti-pesa vyao akaenda-mbali na kusema atahakikisha wanajengewa daraja la Mbutu, matamshi yaliyoleta mashiko kwa wakaazi wa Huko.. tofauti na matamshi aliyoendanao Arumeru mashariki, Benja katumia muda mwingi akijisafisha mwenyewe mbele ya jamii ya wameru na watanzania kwa ujumla kwamba hahodhi ardhi kubwa kama “inavyosemekana” (sijui inasemekana wapi maana mwoga hukimbia hata kivuli chake), lakini pia akaeleza anayo orodha ya watu waliokwiba ardhi na ataipeleka kwako ili uwashughurikie. (kha sasa orodha inapelekwa kwa rais? Yeye Benja kaipatawapi orodha.
Kumbe kuna watu wamekwiba ardhi na yeye anawatambua ila kawakumbatia hadi Leo sa ya kampeni.. hivyo kusingekuwa na kampeni ina maana wangekumbatiwa forever, kama kwenye jimbo moja ana uwezo wa kukumbatia uhaini na Uhalifu(ukabaila) mkubwa kiasi hiki je Tanzania Yote mbaba huyu kakumbatia mangapi??!!) hoja hii mzee ni kama kuishtaki serikali mbele ya wananchi wake kwamba inajua matatizo yao ila kwa maksudi imekumbatia wahalifu na haitaki kuwasaidia wananchi wake.
Benja akaenda mbali kwa kwa kutamka kwamba kiongozi mmojawapo wa kambi ya chama cha upinzani, ambaye ni kiungo muhimu kwanye kampeni  za chama chake huko Arumeru si mwana ukoo wa Juliasi .. Alifanya hivyo makusudi kwa sababu yeye anamjua Vicent, (tena wanajuana fika sitaki niseme zaidi) .. sasa kuropoka mbele ya wananchi waziwazi  vile analenga kuwaamsha watanzania Juu ya Ule uvumi ambao Chama kilitumia Nguvu Nyingi  sana Kuufukia.
Na Uvumi huu ameshauchokonoa na umefunuka sasa, unadhani utauzibaje.. ?? sasa kama hii si hujuma wewe Utaiitaje.? Waandishi wa habari wakim-mwagikia mama Maria , na kumchabanga maswali bibi yetu huyu atajikuta akiongea mambo ambayo chama hakitayabeba siku za Usoni.
Tunaweza tukamlinda kwa sasa ila hatujui siku chama letu likipewa talaka na Watanzania, *kichwa* kitakachoshika dola hatujui kitaamua nini, jamaa wanaweza kumwita bibi ili wamhoji “on Public devote” na akasema kila kitu, unadhani utakuwa wapi wewe.. ona Juzi kati bibi kamtetea Benja kwamba hakumuua Juliasi, na kwamba yeye bibi anajua SIRI, sasa hilo ni swali la Pili,  siri gani bibi yetu huyu  amejikunjia.. watanzania watataka aiweke wazi, hapo.. ???!! kwa Kweli mzee Benja Katumaliza…

Baba wa Taifa, Marehemu Julius Kambarage Nyerere
2.       Kingine Ratiba anaichakachua Sana mwigulu huyu bwana, mtu mbishi na mgomvi sijapata ona .. watu  hawa wana Lao mzee, Kumbuka vikao kadha na masimu kadha wa kadhaa yalitembea usiku kucha kutuliza mashambulizi haya, na tukaazim Mzee Tendwa kwa Rungu alilopewa akemee Kumtamka Marehem Juliasi kwenye kampeni Hizo, But see what happens,Stephen kwa majigambo nae karudia kauli ile le tuliyoikataa, kwamba Nyerere hayuko Upinzani, yeyote aliyeko Upinzania sio Nyerere hata kama katokea ukoo wa Juliasi, wamkatae.. sasa anachokifanya hapa ni kumwagilia zaidi mbegu ile tunayotaka ilale.
Alipoulizwa na Tendwa kwa ubabe alijibu yeye ni wa ukoo wa Juliasi ingawa kwa barua hivyo hakuna kinachomzuia kuongelea juu ya ukoo uliomkubali awe mtoto (ingawa wa mbali-kambo). Stephen ameenda mbali na kuzua hoja ya Uraia wa Siyoi. Sasa ndio amewaamsha wananchi na waliodhani ni uvumi kumbe ni kweli hakuzaliwa kwenye ardhi ya Tanzania, jambo ambalo limezua mstuko wa wananchi wengi hapa.
Akasema Siyoi amezaliwa Kenya kwa sababu wazazi wake walikuwa wanaishi na kufanya kazi huko, jambo ambalo tena limewastua sana wananchi ambao walidhani ni uzushi kumbe kweli. Maneno haya yana maana kwamba damu ya kitovu cha sioi haikumwagika kwenye ardhi ya Meru, hivyo hawezi akawa na uchungu na ardhi ambayo haina damu yake, kitu ambacho kwa wameru na  wazee wa kimila ni mwiko. Amemtukanisha waziwazi mgombea kwa ukoo wake.
Sendeka nae kaja na gia ya Ubaguzi wa kikabila kwamba watu wa Musoma (Mara) wasiwachagulie nani anafaa nani hafai maneno ambayo unakumbuka kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais 1995,  marehemu alikataa kukanyaga zuria la ukumbi mpaka majina kadhaa ya wagombea yaondolewe, na kijivurugu kikatokea na mmoja wa wagombea akaropoka “huyu mtu wa mara akakae Butiama apumzike asituchagulie nani anafaa nani hafai kwani sisi hatuna akili”, .. na kamsemo hako kamerudia kinywani mwa Ole sendeka!!
Kuna Jambo hapa mzee, ni HUJUMA inatembea.. Lusinde na Ole sendeka wameng’ang’ana mpeni kura Siyoi atunze familia kubwa aliyobebeshwa na Babake. Huu ni Upuuzi, yaani Mzee wa watu alikuwa akirundika watoto kwa mategemeo kwamba watalelewa na Mwanae.
Huu mtindo wa kumfanya mtoto kuwa mtaji ulianza wapi.. matamshi haya yana lengo la kuidharau, kuinyanyapaa familia hiyo ya marehemu mbunge wetu kwamba ina njaa, na isipopewa kudra ya mtoto kuwa mbunge basi ndo imekwisha hivyo, lakini pia ni ujumbe kwamba kama uko kwenye Chama letu, na Ukapatwa na Umauti, basi na jina lako linafutika na Chama hakikujui tena hivyo ili kuonekana chama kinajali basi afadhali member mmoja wa familia husika aendelee kuwa kiongozi.. aise Karume, Ali mwinyi, Nape, Shelu na kadhalika pokeeni msg hiyo. Hii yote ni Hujuma.
Kuhusu  Mgombea Siyoi , Ingawa hajui kuongea, na anaonekana mwenye aibuaibu, anaongea akitazama juu,  akisimama kuzungumza mara nyingi anaongelea mambo ambayo nadhani ilimchukua usiku kucha kuyakariri na mara zote anakosea, mara mradi wa maji unaoanzia Ngarenanyuki, badala ya kusema unatokea Ngarenanyuki (manake upo), unasimamiwa na NEMC (mazingira)na pia kasema wanangojea kibali cha TANAPA waendelee na mradi, wakati ambapo TANAPA hawatoi kibali cha maji bali wanaruhusu tu mradi upite kwenye hifadhi ndogo ya Arusha National Park, ambapo Mlima Meru upo, na si kwamba kuna mazingira yatakayoathirika kwa sababu mradi unapita kandokando ya barabara ambayo ipo toka zamani..  Anyway ingawa mgombea anajiumauma meno ila anajikakamua kuelezea hasa kile ambacho wananchi wanakitaka. Ila anvunjwa moyo na timu yake inayosheheni maneno yenye kila viashirio vya kumuhujumu yeye na Chama kwa Ujumla..
mie niwakilishe..
Makala hii imeandaliwa na SALMA2015 na imetoka kwa mara ya kwanza katika mtandao maarufu wa Jamiiforums
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/235753-hujuma-kwa-siyoi-hujuma-kwa-chama.html

Mwanafunzi akilia na Katiba

Johnseverini Mkini
KATIBA ni Sheria Mama ambayo ni mkataba kati ya Mtawala (serkali ) na Raia. Kwa maana halisi ni kwamba, Katiba ni mali ya Raia wa Tanzania ambayo inatoa ufafanuzi kwa Mtawala jinsi ya kufuata taratibu za kumtawala Raia mwenye katiba.

Kwa maana hiyo, Katiba ni mali ya Watanzania wote, na siyo mali ya SERKALI., hivyo basi Serkali inatumia Katiba kuongoza nchi na watu wake bila kwenda kinyume kwa mujibu wa taratibu na, Katiba itumiwe na raia wote bila kuangalia Ukabila, dini, rangi au madaraka.

(ii) Kwa kuwa Katiba ni Sheria Mama, asiweko mtu, au raia kuwa juu ya KATIBA, bali watu wote bila kujali madaraka, watakuwa chini ya Katiba.

(iii) Katiba ni sheria mama ya nchi kwa raia wote, hivyo kwenye katiba mpya, kiondolewe kipengele cha kumkinga Rais kutoshitakiwa pindi anapothibitika kuwa ametenda makosa ya kuvunja katiba anapokuwa madarakani, kwa manufaa binafsi au familia yake, jamaa au rafiki.

Mbali na kushtakiwa kiongozi husika aondolelwe/asimamishwe uongozi mara moja (Impeachment) kwa manufaa ya umma kwa kufuata taratibu.

Mgawanyo wa madaraka ya viongozi kikatiba
Mmiliki wa Katiba:- Kimsingi, Katiba ni mali ya raia wote wa nchi ya Tanzania. (Serkali itaitumia Katiba kama ni moja ya vitendea kazi vyake tu) ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kila raia anafuata sheria na taratibu za nchi,na kila raia anapata haki zake zote za msingi anazostahili, (kwa kifupi, Serkali ni msimamizi mkuu wa kuhakikisha kuwa Katiba inatumika kama ilivyokusudiwa na raia wake wote).

Mahakama:
Mahakama ni chombo (Mhimili huru). Muhimu ambao una majukumu ya kutafsiri sheria zote za nchi zitokanazo na Katiba na zile zinzotungwa Bungeni baada ya kuzingatia Katiba.

Pendekezo:- Mahakama uwe mhimili huru usiofungamana na Serkali ili uweze kutenda haki katika kazi zake za kila siku.
Majaji wa mhimili huo, wasiwe wateule wa Rais, (wachaguliwe na Bunge )na mahakimu wa mikoa na wilaya na mahakama za mwanzo wote wawe waajiriwa wa Mahakama Kuu.

Madaraka ya Rais
Kumekuwapo na utendaji mbovu na usioridhisha wa watumishi wa Serkali wanaoteuliwa na Rais ambaye pia ni mkuu wa nchi, ambapo baadhi ya nyanja muhimu hazileti matokeo mazuri kwenye miradi ya maendeleo ambayo inatengewa fedha na Bunge kama ilivyokusudiwa, kwa kukosa wasimamizi mahiri ambao wengi wao ama wanateuliwa kwa kufahamiana, au kwa urafiki, au kwa kulipwa fadhila lakini hawana uwezo kiutendaji.
Kwa hiyo iko haja ya kupunguza madaraka aliyopewa Rais ya kuteua watendaji kadhaa wa ngazi mbali mbali kitaifa ambao hawana tija kwa jamii, zaidi ya kukilinda chama cha siasa kinachokuwepo madarakani kwa wakati husika.
Kwa mfano:- Uteuzi wa Mkuu wa mkoa (RC) sanjari na RAO kwa ngazi ya mkoa, na DC na DAO kwa ngazi ya wilaya, vyeo ambavyo vilibuniwa na Wakoloni, vikiwa ni daraja la utawala kulinda maslahi ya Gavana kutoka Mikoani na Wilayani. Kwa sasa hivi hatuna wakoloni, hivyo sababu ya kuwa na vyeo hivyo haipo tena, kwa kuwa vyeo hivyo havina tija kabisa kwa walipa kodi na ni ufujaji wa fedha za serkali.
Permanent Secretaries (Makatibu wakuu wa wizara) na wakuu wote wa mashirika ya umma,wote hao ni wateule wa Rais kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakionekana kisiasa zaidi kuliko kuwa watendaji wa serkali kwenye maeneo yao ya kazi na,mara nyingine wakingilia kazi za mtendaji wa Halmashauri za Wilaya na za Miji.
Lakini, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ni mtu anayewasiliana moja kwa moja na raia vijijini, na mijini katika shughuli zote za maendeleo za kila siku. Hata matumizi mabaya ya fedha za miradi husika, anayekaguliwa mahesabu na kuadhibiwa pindi anapobainika kuwa na makosa, ni Mkurugenzi wa Halmashauri, wakati DC na Mkuu wa Mkoa wakiwa nyuma ya pazia hawaonekani, wala hawaguswi. Huo ni uonevu kisiasa.

Pendekezo (a)
Kwa maana hiyo, hakuna haja ya kuwapo vyeo vya, RC, RAO, DC, na DAO kwa hiyo ingefaa vifutwe kama vilivyofutwa vyeo vya RDD na DDD na kubakiza cheo cha DED na watendaji wake wote katika ngazi ya wilaya, ambao Katiba itamke kuwa hao waajiriwe kulingana na taaluma zao. Lakini uwepo utaratibu wa kiutawala wenye kuunganisha madaraka katika nyanja za ulinzi na usalama kazi ambazo zitafanywa na Disrict Executive Director baada ya cheo cha DC kuondolewa.
Pia Taasisi Kupambana na Kuzuia Rushwa, DPP(Mkurugenzi wa Mashtaka) na DIC (Mkurugenzi wa Upelelezi, na Mwanasheria Mkuu wa Serkali (A.G) hawa wameonyesha udhaifu mkubwa sana katika kufanya kazi zao kwa haki hasa inapodhihirika, kuwa Mtuhumiwa anayepaswa kukamatwa, kupelelezwa na kushtakiwa na kuhukumiwa, anatoka sehemu nyeti, au ni mteule wa Rais basi utaona hapo haki ikipindishwa ili kumwokoa mhusika.

Pendekezo (b)
Vyeo hivyo vya TAKUKURU, DPP, DIC na AG viwepo lakini visitokane na uteule wa Rais, ili waweze kufanya kazi yao bila upendeleo, lakini wawe Watanzania wenye taaluma husika na uwezo wa kufanya kazi hizo, waombe kazi na kusailiwa na Bunge, kisha Rais atawaapisha, lakini wote hao watawajibika bungeni.Source: Mwananchi 18/06/2012

KUTOKA CWT


HEBU TIZAMA TOFAUTI HII YA KUTISHA YA VIWANGO VYA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA WA TZ! (Ajira mpya cheti)
Mwl 244,400/= Afya 472,000/= Kilimo/mifugo 959,400/= Sheria 630,000/=


Diploma mwl 325,700/= Afya 682,000/= KLM/MFG 1,133,600/= sheria 871,500/=



degree mwl 469,200/= Afya 802,200/= Klm/MFG 1,354,000/= Sheria 1,166,000/= Je upo tayari kuvumilia kunyanyaswa hivo katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na
mfumuko wa bei wa kutisha? Ungana na Cwt kudai 
nyongeza ya mishahara 100%, Teaching allowance hardship allowance. Wape sms hii 
walimu 20 tu! Mshikamano daima.


CWT yaanza kusambaza ujumbe wa simu (sms) za mgomo kwa walimu nchi nzima

Kinachofurahisha ni kuwa kila mara Walimu huwa wanajiandaa kugoma kisha wananyong'onyea taratibu. Nilipozungumza na baadhi yao kwa nini wakasema huwa wengi wamecheza kanyanga kwenye vyeti kwa hiyo wanajua wakiweka msimamo mchujo ukaanza wataumbuka wengi.

Hata hivyo nashauri kuwa ikiwa umeshasajiliwa, kubwa ni kusimamia haki, haijalishi vitisho ni heri kufa kishujaa. Swali ni kuwa ili kupata watu wa afya, mifugo sheria nk, je wanahitaji waalimu kuwafikisha hapo; ikiwa ndivyo basi waalimu wana mahali pa kuanzia.

Monday, June 18, 2012

YAFAHAMU MAISHA YA LINAH WA THT 

 




















*Baada ya kumwobea Mchungaji atangaza ndoa

ESTERINA Sanga ‘Linah’ jina analofahamika katika sanaa soma makala ya msanii huyu chipikizi mkali ambapo anabainisha mambo mbalimbali yanayomuhusu yeye kama jinsi mtiririko huu unavyokwenda.
MAISHA KABLA YA UIMBAJI Kabla yakuanza uimbaji Linah alikuwa anajishughulisha na uimbaji wa nyimbo za injili lakini sehemu kubwa ya maisha yake ilikuwa ni shule kwa sababu alianza muziki rasmi muda mfupi baada ya kumaliza shule baada na kushindwa kuendelea kutokana na matatizo ya nguvu za giza yaliyompelekea kuwa anapata ukichaa nyakati flaniflani hata kuwa anapelekwa kwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ili amuombee ambapo Mchungaji huyo alitaka kumuoa kwa madai yakuwa nae karibu ili awe anamfanyia maombezi
USHAWISHI WA MUZIKI;Linah alishawishiwa sana kuimba kwa kupitia wasanii kama Lady Jaydee na Banana Zorro kutokana kuwa ni wanamuziki pekee wa kitanzania waliokuwa wanamvutia sana kutokana na kazi zao wanazozifanya.
Pia Linah alishawishiwa sana na baadhi ya rafiki zake wa karibu kubadilisha aina ya muziki aliokuwa anauimba…kutoka nyimbo za dini kwenda nyimbo za kidunia .

KWA MUDA GANI AMEKUWA AKIIMBA?-Ni miaka minne mpaka sasa toka Linah aanze na hii ni kutokea august,2009 baada ya kuchaguliwa kuwa mshindi wa shindano lililoendeshwa na clouds fm ambalo lilikuwa linajulikana kama nyuki star search ambapo wimbo wake wa kwanza kuiimba na ambao ulimtambulisha ni ‘atatamani’ ulioandikwa na Amini pamoja na Ruge Mutahaba.
WAJUE WASHIRIKA WA KARIBU WA LINAH KIMUZIKI

Linah anafanya kazi kwa ukaribu kabisa na wanafunzi wote wa T.H.T.ikiwemo Amini,Barnaba,Mwasiti na Ditto.
-Mbali na hao pia hufanya kazi na wasanii nje ya T.H.T ambao ni Banana Zahir Zorro,lady Jaydee na Black.
MBALI NA MUZIKI

Mbali na muziki Linah pia anafanya uigizaji kwani kwa sasa amesaini mkataba wa na clods Tv wa kuigiza series inayokwenda kwa jina la 69 Records ambayo itakuwa inarushwa na Clouds Tv.
Njozi zake nje ya muziki ni kuwa mbunifu wa mitindo ya mavazi huo ndiyo mpango wake ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za mitindo kwa ujumla ikiwa ni katika kujiongezea kipato na kupunguza utegemezi wa muziki pekee katika kuendesha maisha yake.
Nyota anayemvutia nche ya nchi ni nchi Christina Millan kutokana na yeye mwenyewe kumwelezea kama mwanamuziki wanayefanana naye katika ‘life style’.
Linah anasema anaishi peke yake yake maeneo ya Kinondoni ,Dar es Salaam ambalko amepanga chumba kimoja tu.
-Muda si mrefu lina anatarajia kupokea gari lake aliloliagiza kutoka nje ya nchi.
-Mara nyingi nyakati za weekend Linah huwa anapendelea sana kutembelea maeneo ya wet ‘n’world kutokana na ukweli kuw
Linah anapenda sana kuogelea.
JINA;Estellina Peter Sanga
KABILA ;Mkinga kutoka Iringa
TAREHE YA KUZALIWA;17/3/1990
MAHALI ALIPOZALIWA;Hospitali ya Muhimbili,Dar es Salaam

ELIMU YAKE;
1998-2003 elimu ya msingi…….Ubungo Msewe shule ya msingi
2004-2008 Kidato cha kwanza mpaka cha nne……Msigani sekondari.
2009,Kwa wiki mbili mafunzo ya komputa University Computing
Center(UCC)

ALBAMU YAKE;
Albamu yake ya kwanza ilikuwa inakwenda kwa jina la ‘Ninakukimbila’ ilikuwa yenye nyimbo 10 za dini ambapo nyimbo hizo alitengenezewa na kaka yake ambaye alikuwa anamiliki studio ya kurekodia nyimbo za dini, ingawa mwisho wa siku albamu hiyo haikutoka.
Kwa sasa ana albamu yake nyimbo zenye mahadhi ya Afro pop, Zouk ,Reggae anayotarajia kuitoa mwakani ndani ya album hiyo kutakuwa na nyimbo kama ‘Maneno Maneno’ aliyomshirikisha Banana Zorro, Lonely, Bora Nikimbie,Atatamani, Chozi Langu na yingine nyingi alizodai kuwa zitakuwa moto wa kuotea mbali.
KUHUSU FAMILIA YAKE
Familia ya Linah ni familia ya kidini kutokana na ukweli kuwa baba mzazi wa Linah ni Mchungaji wa Kanisa .
Familia yake ina jumla ya watoto watano wakati Linah akiwa mtoto wa tatu kuzaliwa kutoka kwenye familia ya Mchungaji Sanga.
-Familia anayotoka Linah ni familia iliyojaa wanafamilia waliojaa vipaji vya vya uimbaji.
Anasema Dada yake mkubwa ni Fortunata ,ameolewa na ana watoto watatu, Angela,ameolewa na ana mtoto mmoja,Linah,,Isaack…..amemaliza kidato cha nne ana uwezo mkubwa wa kupiga ‘Drums’ na Rachel ambaye ni mdogo wake wa mwisho anasoma kidato cha kwanza.
MAISHA YAKE BINAFSI

Linah ana boyfriend ambaye ni mwana muziki pia na jina lake ni Amini.
LINAH YUPO CHINI YA LABEL GANI?-Linah hayupo chini ya label yoyote ile bali yeye ni mwanafunzi wa Tanzania House of Talent(T.H.T) ambayo humsaidia katika kumpatia mafunzo ya kimuziki pamoja na kumsaidia katika michakato yote ya utungaji wa muziki wake sanjari na kurekodi na hatimaye kumsaidia katika kuutangaza.

MIPANGO YA BAADAE YA LINAH KIMUZIKI.-Mpango mkubwa na wa kwanza wa linah ni kurudi shule,na hii ni kutokana na ukweli kuwa yeye aliishia kidato cha nne tu,jambo lililochangiwa kwa kiasi kikubwa na matatizo yake ya kiafya yaliyoelezwa hapo juu.Linah ana mpango pia wa kukuza muziki wake na malengo yake ni kuufanya ujulikane Afrika nzima na Duniani kote.-Linah ana mpango wa kutoa albamu yake January 2011.

TETESI ZA MJINI
-Linah aliwahi kukumbwa na skendo ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Roma …’sijawahi hata kukutana na Roma ‘Linah alisema
-‘mimi ni mpole sana na ninaelewena karibu na watu wote lakini mtu huwa akiniingilia katika maswala yangu binafsi huwa nawahi sana kukasirika na kulia na huwa ninakasirika zaidi pale anapokuja mtu na kuniuliza sababu ya kulia’ anasema Linah.