Tuesday, June 19, 2012

KUTOKA CWT


HEBU TIZAMA TOFAUTI HII YA KUTISHA YA VIWANGO VYA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA WA TZ! (Ajira mpya cheti)
Mwl 244,400/= Afya 472,000/= Kilimo/mifugo 959,400/= Sheria 630,000/=


Diploma mwl 325,700/= Afya 682,000/= KLM/MFG 1,133,600/= sheria 871,500/=



degree mwl 469,200/= Afya 802,200/= Klm/MFG 1,354,000/= Sheria 1,166,000/= Je upo tayari kuvumilia kunyanyaswa hivo katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na
mfumuko wa bei wa kutisha? Ungana na Cwt kudai 
nyongeza ya mishahara 100%, Teaching allowance hardship allowance. Wape sms hii 
walimu 20 tu! Mshikamano daima.


CWT yaanza kusambaza ujumbe wa simu (sms) za mgomo kwa walimu nchi nzima

Kinachofurahisha ni kuwa kila mara Walimu huwa wanajiandaa kugoma kisha wananyong'onyea taratibu. Nilipozungumza na baadhi yao kwa nini wakasema huwa wengi wamecheza kanyanga kwenye vyeti kwa hiyo wanajua wakiweka msimamo mchujo ukaanza wataumbuka wengi.

Hata hivyo nashauri kuwa ikiwa umeshasajiliwa, kubwa ni kusimamia haki, haijalishi vitisho ni heri kufa kishujaa. Swali ni kuwa ili kupata watu wa afya, mifugo sheria nk, je wanahitaji waalimu kuwafikisha hapo; ikiwa ndivyo basi waalimu wana mahali pa kuanzia.

No comments:

Post a Comment