TRIPOLI YAANGUKA; MWISHO WA GADDAFI?
Ndani
ya masaa 72 Jiji la Tripoli nchini Libya limeanguka mikononi mwa waasi
ambao walikuwa wanaendesha kampeni ya kumuondoa rais wa nchi hiyo
Dikteta Muammar Gaddafi. Kuanguka kwa jiji la Tripoli kunaashiria
kuhitimishwa kwa kampeni hiyo iliyozidi kwa miezi sita kamili sasa na
ambayo imegharimu maisha ya mamia ya wananchi wa Libya ambao wamekuwa
chini ya utawala wa Gaddafi na familia yake kwa zaidi ya miaka 40 sasa.
Mwishoni mwa juma waasi wa Libya walikuwa wanalizunguka jiji hilo la
Afrika ya Kaskazini kama fundo la kamba na pole pole waliteka maeneo
mbalimbali na kuzima majaribio yoyote ya utetezi wa wapiganaji wa
Gaddafi. Kusika siku ya Jumamosi jioni kuamkia Jumapili waasi walikuwa
kilomita chache kutoka Viwanja vya Kijani ambapo wiki kadha wa kadha
mashabiki wa Gaddafi walikuwa wakikutana kutiana shime.
Maelfu ya wananchi wa Libya wakipepea bendera ya waasi – ambayo ni
bendera ya zamani ya Mfalme wa Libya – walianza kujitokeza barabarani
kuwapokea waasi hao na usiku wa kuamkia Jumatatu hii maelfu zaidi
wamejitokeza katika mitaa na viunga vya Jiji la Tripoli kuwakaribisha
waasi hao ambao wanapigana chini ya uongozi wa Baraza la Mpito la Libya
ambalo linawakilisha serikali mbadala ya ile ya Gaddafi. Hadi hivi sasa
nchi 32 zimetambua baraza hilo kuwa mwakilishi halali wa wananchi wa
Libya. Tanzania siyo mojawapo. (more…)
No comments:
Post a Comment