Prince Charles kutembelea Tanzania Nov 6
Mwana
wa Malkia wa Uingereza – Prince Charles of Wales – anatarajiwa
kutembelea Tanzania kuanzia Jumapili akitokea Afrika ya Kusini ambako
ameanza ziara ya siku nane katika bara la Afrika. Prince Charles ambaye
ni mrithi wa kiti cha ufalme wa Uingereza ni mtoto wa kwanza wa Malkia
Elizabeth wa Pili.
Katika ziara yake hiyo Prince Charles ameambatana na mkewe Duchess of
Cornwell Camilla Parker. Ziara ya Tanzania itaanza tarehe 6 hadi tarehe
9 na ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Tanganyika (eneo la Tanzania Bara) ilipata uhuru wake kutoka Uingereza
iliyokuwa inaitawala kwa agizo la Umoja wa Mataifa ambapo Uingereza
ilitakiwa iiandae Tanganyika kuwa huru.
Mara ya mwisho kwa Prince Charles kutembelea Tanzania katika ziara
rasmi ilikuwa ni 1984 na Bi. Parker hajawahi kutembelea Tanzania. Prince
Charles ndiye baba yao Prince William na Prince Harry na mke wake wa
kwanza Princess Diana (mama yao William na Harry) alikufa katika ajali
ya gari mwaka 1997.
No comments:
Post a Comment