Tuesday, June 19, 2012

HUJUMA kwa Siyoi Arumeru…. Hujuma kwa Chama chetu

Mzee Salaam,
Najua huwa unapitia hapa ukikwanguiwa kule Facebook, au “Mtuitui” anakujuza yanayoendelea, ila mchunge sana, ni mnafiki huwa anakumwagia porojo na umbeaumbea tu sanasana siku akiwa anasaka pesa za kujirusha. Mie sichapi umbea ..maa yake hawachelewi sema weka source.. source si ndio hii hapa au wewe unataka ipi tena..we-mbaba unamambo..!!
Mzee unakumbuka kilipotemwa kikao cha KK cha mwisho na kwa  rungu tukagandamizia Siyoi for Arumeru, Siyoi for the Party, na baadae ukapokea msg kutoka kwa “kiraka” kwamba MC alikuwa anachonga mbovu nje ya kikao kwamba kwa mtaji huu ni bahati kushika nafasi ya pili au tatu kwa chama letu kwenye kinyang’anyiro hicho cha Ubunge, huko kwa Wameru kutokana na sababu walizozungumzia zungumzia wajumbe za vijiubabe, vijiubabe na kama kuburuzana flan-hivi, dhana iliyookea kule Dodoma wakati wa kupitisha ile karata ya mabadiliko ya katiba ……… ila ukapuuzia kamsemo kake, nadhani sasa kuna sababu ya kuanza Tathimini kwanini Tumeshindwa.
Werevu hawasubiri mavuno ndipo wafanye tathimini, wapumbavu husubiri hadi nukta ya mwisho ya tone la mvua ndipo huamka kwamba mwaka huu ni wa njaa na kukurupuka kuomba msaada.
Kuna Uzi unatembea Chini kwa Chini wa Kukiangamiza Chama, ni HUJUMA iliyokamilika yenye Lengo la Kukomoana na kulipizana Visasi. Ukweli usemwe hata kama unauma.. look here..
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye ndiye aliyezindua kampeni za CCM Arumeru Mashariki
1.       Wakati Benja akifungua kampeni, kule Igunga alielezea kwa madaha jinsi Serikali kupitia chama letu ilivyoleta maendeleo ya miundombinu ya Barabara, Toka Dar hadi Igunga ni lami, Chama letu limefanikisha kufungua matawi ya benki (NMB) Igunga ambapo sasa wananchi wanaweza kukopa na kuweka vijisenti-pesa vyao akaenda-mbali na kusema atahakikisha wanajengewa daraja la Mbutu, matamshi yaliyoleta mashiko kwa wakaazi wa Huko.. tofauti na matamshi aliyoendanao Arumeru mashariki, Benja katumia muda mwingi akijisafisha mwenyewe mbele ya jamii ya wameru na watanzania kwa ujumla kwamba hahodhi ardhi kubwa kama “inavyosemekana” (sijui inasemekana wapi maana mwoga hukimbia hata kivuli chake), lakini pia akaeleza anayo orodha ya watu waliokwiba ardhi na ataipeleka kwako ili uwashughurikie. (kha sasa orodha inapelekwa kwa rais? Yeye Benja kaipatawapi orodha.
Kumbe kuna watu wamekwiba ardhi na yeye anawatambua ila kawakumbatia hadi Leo sa ya kampeni.. hivyo kusingekuwa na kampeni ina maana wangekumbatiwa forever, kama kwenye jimbo moja ana uwezo wa kukumbatia uhaini na Uhalifu(ukabaila) mkubwa kiasi hiki je Tanzania Yote mbaba huyu kakumbatia mangapi??!!) hoja hii mzee ni kama kuishtaki serikali mbele ya wananchi wake kwamba inajua matatizo yao ila kwa maksudi imekumbatia wahalifu na haitaki kuwasaidia wananchi wake.
Benja akaenda mbali kwa kwa kutamka kwamba kiongozi mmojawapo wa kambi ya chama cha upinzani, ambaye ni kiungo muhimu kwanye kampeni  za chama chake huko Arumeru si mwana ukoo wa Juliasi .. Alifanya hivyo makusudi kwa sababu yeye anamjua Vicent, (tena wanajuana fika sitaki niseme zaidi) .. sasa kuropoka mbele ya wananchi waziwazi  vile analenga kuwaamsha watanzania Juu ya Ule uvumi ambao Chama kilitumia Nguvu Nyingi  sana Kuufukia.
Na Uvumi huu ameshauchokonoa na umefunuka sasa, unadhani utauzibaje.. ?? sasa kama hii si hujuma wewe Utaiitaje.? Waandishi wa habari wakim-mwagikia mama Maria , na kumchabanga maswali bibi yetu huyu atajikuta akiongea mambo ambayo chama hakitayabeba siku za Usoni.
Tunaweza tukamlinda kwa sasa ila hatujui siku chama letu likipewa talaka na Watanzania, *kichwa* kitakachoshika dola hatujui kitaamua nini, jamaa wanaweza kumwita bibi ili wamhoji “on Public devote” na akasema kila kitu, unadhani utakuwa wapi wewe.. ona Juzi kati bibi kamtetea Benja kwamba hakumuua Juliasi, na kwamba yeye bibi anajua SIRI, sasa hilo ni swali la Pili,  siri gani bibi yetu huyu  amejikunjia.. watanzania watataka aiweke wazi, hapo.. ???!! kwa Kweli mzee Benja Katumaliza…

Baba wa Taifa, Marehemu Julius Kambarage Nyerere
2.       Kingine Ratiba anaichakachua Sana mwigulu huyu bwana, mtu mbishi na mgomvi sijapata ona .. watu  hawa wana Lao mzee, Kumbuka vikao kadha na masimu kadha wa kadhaa yalitembea usiku kucha kutuliza mashambulizi haya, na tukaazim Mzee Tendwa kwa Rungu alilopewa akemee Kumtamka Marehem Juliasi kwenye kampeni Hizo, But see what happens,Stephen kwa majigambo nae karudia kauli ile le tuliyoikataa, kwamba Nyerere hayuko Upinzani, yeyote aliyeko Upinzania sio Nyerere hata kama katokea ukoo wa Juliasi, wamkatae.. sasa anachokifanya hapa ni kumwagilia zaidi mbegu ile tunayotaka ilale.
Alipoulizwa na Tendwa kwa ubabe alijibu yeye ni wa ukoo wa Juliasi ingawa kwa barua hivyo hakuna kinachomzuia kuongelea juu ya ukoo uliomkubali awe mtoto (ingawa wa mbali-kambo). Stephen ameenda mbali na kuzua hoja ya Uraia wa Siyoi. Sasa ndio amewaamsha wananchi na waliodhani ni uvumi kumbe ni kweli hakuzaliwa kwenye ardhi ya Tanzania, jambo ambalo limezua mstuko wa wananchi wengi hapa.
Akasema Siyoi amezaliwa Kenya kwa sababu wazazi wake walikuwa wanaishi na kufanya kazi huko, jambo ambalo tena limewastua sana wananchi ambao walidhani ni uzushi kumbe kweli. Maneno haya yana maana kwamba damu ya kitovu cha sioi haikumwagika kwenye ardhi ya Meru, hivyo hawezi akawa na uchungu na ardhi ambayo haina damu yake, kitu ambacho kwa wameru na  wazee wa kimila ni mwiko. Amemtukanisha waziwazi mgombea kwa ukoo wake.
Sendeka nae kaja na gia ya Ubaguzi wa kikabila kwamba watu wa Musoma (Mara) wasiwachagulie nani anafaa nani hafai maneno ambayo unakumbuka kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais 1995,  marehemu alikataa kukanyaga zuria la ukumbi mpaka majina kadhaa ya wagombea yaondolewe, na kijivurugu kikatokea na mmoja wa wagombea akaropoka “huyu mtu wa mara akakae Butiama apumzike asituchagulie nani anafaa nani hafai kwani sisi hatuna akili”, .. na kamsemo hako kamerudia kinywani mwa Ole sendeka!!
Kuna Jambo hapa mzee, ni HUJUMA inatembea.. Lusinde na Ole sendeka wameng’ang’ana mpeni kura Siyoi atunze familia kubwa aliyobebeshwa na Babake. Huu ni Upuuzi, yaani Mzee wa watu alikuwa akirundika watoto kwa mategemeo kwamba watalelewa na Mwanae.
Huu mtindo wa kumfanya mtoto kuwa mtaji ulianza wapi.. matamshi haya yana lengo la kuidharau, kuinyanyapaa familia hiyo ya marehemu mbunge wetu kwamba ina njaa, na isipopewa kudra ya mtoto kuwa mbunge basi ndo imekwisha hivyo, lakini pia ni ujumbe kwamba kama uko kwenye Chama letu, na Ukapatwa na Umauti, basi na jina lako linafutika na Chama hakikujui tena hivyo ili kuonekana chama kinajali basi afadhali member mmoja wa familia husika aendelee kuwa kiongozi.. aise Karume, Ali mwinyi, Nape, Shelu na kadhalika pokeeni msg hiyo. Hii yote ni Hujuma.
Kuhusu  Mgombea Siyoi , Ingawa hajui kuongea, na anaonekana mwenye aibuaibu, anaongea akitazama juu,  akisimama kuzungumza mara nyingi anaongelea mambo ambayo nadhani ilimchukua usiku kucha kuyakariri na mara zote anakosea, mara mradi wa maji unaoanzia Ngarenanyuki, badala ya kusema unatokea Ngarenanyuki (manake upo), unasimamiwa na NEMC (mazingira)na pia kasema wanangojea kibali cha TANAPA waendelee na mradi, wakati ambapo TANAPA hawatoi kibali cha maji bali wanaruhusu tu mradi upite kwenye hifadhi ndogo ya Arusha National Park, ambapo Mlima Meru upo, na si kwamba kuna mazingira yatakayoathirika kwa sababu mradi unapita kandokando ya barabara ambayo ipo toka zamani..  Anyway ingawa mgombea anajiumauma meno ila anajikakamua kuelezea hasa kile ambacho wananchi wanakitaka. Ila anvunjwa moyo na timu yake inayosheheni maneno yenye kila viashirio vya kumuhujumu yeye na Chama kwa Ujumla..
mie niwakilishe..
Makala hii imeandaliwa na SALMA2015 na imetoka kwa mara ya kwanza katika mtandao maarufu wa Jamiiforums
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/235753-hujuma-kwa-siyoi-hujuma-kwa-chama.html

No comments:

Post a Comment